Abbey
Abbey | Benedictine Abbey Ndanda
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Wabenediktini Wamisionari

Abasia ya Ndanda ni kati ya abasia ambazo kwa pamoja zinatengeneza shirika la kimataifa la Wabenediktini Wamisionari wa Mt. Ottilia (Congregatio Ottiliensis OSB). Nyumba mama pamoja na ofisi kuu ya shirika zipo Bavaria, Ujerumani. Habari zaidi juu ya shirika letu zinapatikana kwa kutembelea tovuti hii: Soma Zaidi >>>

Utume wetu Msumbiji

Misioni mpya ya Mecúa, katika jimbo kuu la Nampula, ilianza mwaka 2022. Hii ilikuwa hasa ni kuhamishwa kwa misioni ya N’nango kutoka jimbo la Pemba, ambayo ililazimika kuhamishwa kutokana na sababu za kiusalama. Jumuiya hii inaundwa na ndugu wanne. Wengine badowanaendelea na masomo yao ya kiteolojia nchini Tanzania: Soma Zaidi >>>

Monasteri ya Mwenye Heri Isidori Bakanja, Dodoma

Kusoma alama za nyakati ni mojawapo ya vipengele muhimu kwa kila shirika la kimisionari. Kuhamishwa kwa shughuli za kiutawala kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kama mji mkuu mpya, hakukuleta tu mabadiliko katika uwanja wa kisiasa wa Tanzania, bali pia katika Kanisa. Dodoma ilijikuta ikipokea wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Makanisa, shule, barabara na taasisi nyingine za kijamii ambazo hapo awali zilionekana kuwa za kutosha, zilijikuta hazitoshelezi kuhudumia idadi kubwa ya watu waliokuwa wakimiminika kutoka kila kona ya
Tanzania: Soma Zaidi >>>