Abbey / Jumuiya / Nyumba Zetu
JUU kabisa katika milima ya Usambara – kadiri ya mwinuko wa mita 2000 kutoka usawa wa bahari ndipo ilipo jumuiya yetu ndogo ya Sakharani. Sakharani ni mahali pazuri kwa shughuli za kilimo na ufugaji. Mazao mbalimbali kama migomba, maparachichi, makademia na mboga za aina mbalimbali zinastawi kwa wingi. Maelfu ya miti pia imepandwa na inaendelea kupandwa katika shamba hili kubwa. Cha pekee, lakini ni kilimo cha zabibu. Ingawa divai yetu haijulikani sana Sakharani Wine (nyeupe na nyekundu) ni divai inayopendwa na wageni wetu na pia mahoteli yaliyoko katika ujirani mwetu. Pamoja na shughuli zingine za kimalezi, Sakharani inatoa fursa kwa yoyote ambaye angependa kufanya likizo , kutulia, kusali na kutembea katika milima mizuri ya Usambara.
JUMUIYA YA KURASINI, DAR ES SALAAM
Jumuiya ya Kurasini ni ndogo kwa maana ya idadi ya ndugu wanaoishi pale ambao kwa kawaida ni wawili tu. Nyumba hii inashughulika na mambo mawili makubwa. Kwanza ni nyumba ya wageni – hasa wale wanaohusiana na watawa au kazi zetu za kimisionari. Kazi nyingine zinazofanyika katika nyumba hii ni zile za kiprokura – yaani kuangalia upatikanaji wa mahitaji mbalimbali kwa ajili ya shughuli zetu za kimisionari.
Benedictine Fathers’ Kurasini,
Kilwa, Road Benderea Tatu,
P.O. BOX 274
Dar es Salaam –
Email: bakanjamkenda@gmail.com
Tel. +255 784 946 519
Kwa habari Zaidi tazama “N’nango, Msumbiji.“