Abbey / Utunzaji wa mazingira / Utunzaji wa Vyanzo vya Maji
NDANDA IMEBARIKIWA kuwa na vyanzo mbalimbali vya maji safi. Tukitambua kuwa „Maji ni Uhai” tunahakikisha kuwa eneo lote ambao chemechemi za maji zinapatikana zinatunzwa kwa gharama yoyote ile. Hii ni kuhakikisha kuwa misitu ya asili iliyoko jirani inalindwa na kwamba hakuna shughuli yoyote ya kibinadamu inafanyika katike eneo hilo. Juhudi hizi zinafanyika, si tu kwa ajili ya kukihakikishia kizazi chetu hiki maji ya kutosha, bali pia kuhakiksha kuwa vizazi vijavyo vitaendelea kufurahia maji ambayo sisi nasi tuliyakuta.