Abasia
Sisi ni akina Nani | Abasia

Sisi ni akina Nani?

Sisi ni akina Nani?

Abbey / Jumuiya / Sisi ni akina Nani

KWANZA KABISA tukukaribishe ndugu mpendwa katika tovuti yetu. Ingawa Wabenediktini wamekuwa kati ya Wamisionari wa kwanza kabisa kuinjilisha Tanzania, hawajulikani sana hasa sehemu ya kaskazini mwa nchi yetu. Hii ni kwa sababu shirika limejikita zaidi eneo la kusini mwa Tanzania. Sisi ni watawa wamonaki ambao tunaishi kadiri ya kanuni ya Mt. Benedikto. Lengo letu kuu ni kumfuata Yesu Kristu katika Maisha ya jumuiya: kusali na kufanya kazi pamoja. Kazi tunazofanya zinalenga kumwendeleza mtawa mwenyewe na jamii inayotuzunguka – katika nyanja zote za kiroho na za kijamii. Ni matumaini yetu kuwa kwa njia ya tovuti hii utaweza kulifahamu shirika letu pamoja na shughuli zake za kimisionari hapa nchini na hata nje ya nchi yeti.  Karibu sana!