Abasia
Duka la Vitabu | Abasia

Duka la Vitabu

Duka la Vitabu

Abbey / Kazi Zetu / Duka la Vitabu

IDARA HII inayoitwa “Bookshop” hakika ni zaidi ya vitabu. Ni kweli kwamba vitabu vinavyochapishwa na NMP vinauzwa katika duka hili. Hii ni pamoja na vitabu vinavyochapishwa na wachapishaji wengine wa ndani au wale wa nje ya nchi. Hata hivyo idara hii inashughulika hasa na uhariri wa vitabu. Hii ni kusema kwamba, kabla miswada haijapelekwa kiwandani kuchapwa, ni lazima ipitie kwanza idara hii ya “publishing.” Ni baada tu ya kupitishwa na idara hii mswada unaweza kuchapishwa. Baada ya kuchapishwa kitabu kitarudi tena katika idara hii – au kuuzwa dukani au kwa ajili ya kusafirishwa kwa wanunuzi wa mbali.