Abasia
Uchungaji | Abasia

Uchungaji

Uchungaji

Abbey / Umisionari / Uchungaji

HATA baada ya Kanisa mahalia kuwa chini ya askofu wa jimbo na mapadre wake, jumuiya ya abasia imekuwa inaendelea kushiriki na kutoa mchango mkubwa katika uchungaji. Wakati kimsingi mtindo wetu wa kuishi umeendelea kuwa wa pamoja katika jumuiya, bado baadhi yetu wanashiriki kikamilifu katika kazi za kuendesha parokia katika majimbo ya Tanga, Mtwara na Lindi. Hii inawawezesha wachungaji wetu kuwaongoza, kuwafundisha na kuwasindikiza watoto, vijana, wanandoa, wagonjwa na wale wote ambao wanahitaji huduma yoyote ya kiroho.