Abasia
Bwawa la Umeme | Abasia

Bwawa la Umeme

Bwawa la Umeme

Abbey / Utunzaji wa mazingira / Bwawa la Umeme

SIKU HIZI  kumekuwa na mawazo tofauti-tofauti kuhusu ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme. Baadhi ya wana-mazingira wanadai kuwa mabwawa hayo yanaharibu mazingira na kutishia maisha ya viumbe. Hili ni jambo linaloweza kutazamwa na kujadiliwa, kwani mazingira ya mabwawa ni tofauti-tofauti. Jambo moja ni la uhakika: umeme unaozalishwa kwa njia ya maji ni rafiki mara dufu kwa mazingira kuliko ule unaozalishwa kwa nguvu za atomiki, dizeli au makaa ya mawe. Kwa kuachana na matumizi ya majenereta makubwa ya dizeli na kutumia umeme wa maji, kutoka bwawa letu dogo, tunachangia katika kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa ambayo inasababisha kuongezeka kwa joto katika sayari yetu.