Abasia
Useremala | Abasia

Useremala

Useremala

Abbey / Kazi zetu / Useremala

IDARA YA USEREMALA imekuwepo tangu misioni ya Ndanda ilipoanza zaidi ya miaka mia moja iliyopita. Hatua kwa hatua idara hii imekua na kuboreshwa. Aina zote za samani zinaweza kuagizwa na kutengenezwa na idara hii. Watu binafsi, mashrika yasiyo ya kiserikali, idara za kiserikali na makanisa – wote wamekuwa wanaagiza samani kutoka idara hii. Kitengo kingine ndani ya useremala kinahusika na masuala ya ujenzi kama kupaua mapaa, n.k. Idara ya useremala ni kati ya idara ambazo licha ya kuwapa ajira watu wengi, inatoa nafasi ya mafunzo kwa vijana mbalimbali. Katika sehemu ya picha ya tovuti hii utaweza kujionea mifano michache ya samani zetu.