Abbey
Bakanja Monastery | Abbey

Monasteri ya Mwenye Heri Isidori Bakanja, Dodoma

Abbey / Monasteri ya Mwenye Heri Isidori Bakanja, Dodoma
Kusoma alama za nyakati ni mojawapo ya vipengele muhimu kwa kila shirika la kimisionari. Kuhamishwa kwa shughuli za kiutawala kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kama mji mkuu mpya, hakukuleta tu mabadiliko katika uwanja wa kisiasa wa Tanzania, bali pia katika Kanisa. Dodoma ilijikuta ikipokea wageni wengi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Makanisa, shule, barabara na taasisi nyingine za kijamii ambazo hapo awali zilionekana kuwa za kutosha, zilijikuta hazitoshelezi kuhudumia idadi kubwa ya watu waliokuwa wakimiminika kutoka kila kona ya Tanzania.

Abasia ya Ndanda ilichukulia hili kama fursa ya kimisionari. Mnamo Desemba 2023, Askofu Mkuu wa Dodoma – Mha. Beautus Kinyaiya, OfmCap – aliweka jiwe la msingi ya Misheni ya Wabenediktini katika kijiji cha Nzinje, karibu na Michese, takriban kilomita 14 kutoka katikati ya jiji kuelekea Kusini Magharibi. Baraka ya Askofu Mkuu katika siku ya kwanza ya mradi huu ilikuwa chanzo cha baraka nyingine nyingi. Ndani ya mwaka mmoja, jengo la monasteri kwa ajili ya ndugu wanne lilikuwa tayari kwa makazi. Kundi la kwanza la ndugu walihamia mnamo Septemba 2024 kuanza maisha mapya ya ora et labora – yaani SALA NA KAZI huko
Dodoma.

Kwa sasa, jumuiya inatekeleza mradi wa shule ya wavulana itakayojulikana kama ABBEY SECONDARY SCHOOL DODOMA. Shule hii itakuwa ya kumbukumbu kwa mwanzilishi wa Wamisionari Wabenediktini – Padre Andreas Amrehein. Shule inatarajiwa kuanza kazi mwezi Novemba 2025. Ndugu pia wamekabidhiwa parokia ya Michese pamoja na vigango vyake kadhaa. Hii ni misioni inayokua kwa kasi – sawa kabisa na miti 10,000 iliyopandwa katika eneo la ekari 56 – ambayo nayo inakuwa
kwa kasi kubwa.

Switzerland:

Missionsprokura der Abtei St. Otmarsberg. Tel. +41 (0) 55 285 8111
Email: abtei@otmasberg.ch

Germany:

United States

Benedictine Mission House in Schuyler, NE: Tel. +1 402 352 2177
Email: missionoffice@benedictinemissionhouse.com