Abasia
Upandaji Miti | Abasia

Upandaji Miti

Upandaji Miti

Abbey / Utunzaji wa mazingira / Upandaji Miti

KILIO KIKUBWA kilichopo duniani siku hizi ni uharibifu wa mazingira na kwa namna ya pekee uharibifu wa misitu. Misitu ambayo hutoa mchango mkubwa katika kuhifadhi na kurekebisha hali ya hewa iko hatarini ulimwenguni kote. Tatizo la kuongezeka joto ulimwenguni husababishwa na uharibifu wa mazingira. Hakika hatuwezi kuyalazimisha mataifa makubwa waache mara moja viwanda vyao ambavyo vinatoa hewa ya ukaa inayotibua hali ya hewa. Hata hivyo tunaweza kuotesha miti; miti ambayo si tu itafyonya hewa hiyo ya ukaa, bali pia itachangia kutunza udongo na maji. Misiti yetu yenye maelfu na maelfu ya miti inachangia katika eneo letu kwa namna kubwa katika kutunza mazingira. Si ajabu, basi, kwamba mara mbili tumepata tuzo ya kitaifa ya utunzaji mazingira.