Abasia
Uchongaji wa Mawe | Abasia

Uchongaji wa Mawe

Uchongaji wa Mawe

Abbey / Kazi Zetu / Uchongaji wa Mawe

SIYO WATU WENGI wanajua sehemu ambapo karakana hii inapatikana. Labda ni kwa sababu karakana hii iko mbali na eneo zilizopo karakana zetu zigine. Hata hivyo, kazi nzuri zinazotokana na karakana hii zinaonekana katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa kutumia aina ya mawe (marble) yanayopatikana jirani na Ndanda, karakana hii inaweza kutengenzeka mambo mbalimbali. Baadhi ya bidhaa zinazotokana na karakana hii ni pamoja na altare, viti vya mawe vya kukalia altareni, visima vya ubatizo, sanamu mbalimbali, mbao za mawe kwa ajili ya matangazo, mawe ya makaburii, n.k. Mfano mzuri wa bidhaa za karakana hii ni kiti cha kiaskofu kinachopatikana katika Kanisa Kuu la Mt. Joseph, Dar es Salaam.