Abasia
Mradi wa Maji ya Kunywa | Abasia

Mradi wa Maji ya Kunywa

Mradi wa Maji ya Kunywa

Abbey / Kazi zetu / Mradi wa Maji ya Kunywa

ABBEY SPRINGS ™ ni mradi mpya na wa kisasa zaidi tulio nao. Ni baraka kubwa tuliyo nayo kwamba Ndanda daima ina maji mengi, safi, salama na ya kutosha. Kutokana na wingi na uzuri wa maji haya, kumekuwepo kwa muda mrefu mawazo ndani ya jumuiya ni kwa namna gani tungeweza kuwashirikisha watu wengine maji haya. Miaka michache ya nyuma tulianza kujaza maji katika chupa kwa kutumia mashine ndogo zilizoendeshwa kwa mikono. Kutokana na kupanuka kwa mahitaji, jumuiya yetu iliamua kuwekeza katika mitambo ya kisasa zaidi. Kwa sasa maji ya Abbey Springs ™ yanazalishwa kwa wingi na kusambazwa maeneo mbalimbali. Maji haya hujazwa katika chupa zenye ujazo wa lita 1.5; lita 1.0 na pia nusu lita (0.5 L). Iwe kwa matumizi yako binafsi, familia, ofisi au kwa ajili ya matukio na sherehe – maji ya Abbey Springs ™ ni chaguo la kuaminika na utakaloweza kulifurahia daima.