Abbey
Utume wetu Msumbiji Mecua | Abbey
Utume wetu Msumbiji
Utume wetu Msumbiji
Abbey / Utume wetu Msumbiji
Misioni mpya ya Mecúa, katika jimbo kuu la Nampula, ilianza mwaka 2022. Hii ilikuwa hasa ni kuhamishwa kwa misioni ya N’nango kutoka
jimbo la Pemba, ambayo ililazimika kuhamishwa kutokana na sababu za kiusalama. Jumuiya hii inaundwa na ndugu wanne. Wengine bado
wanaendelea na masomo yao ya kiteolojia nchini Tanzania.

Baada ya kukamilika kwa monasteri yao ndogo mnamo Desemba 2024, jumuiya inaishi maisha ya Kibenediktini ya sala na kazi. Wakati huo huo, wanatoa huduma ya kichungaji katika vigango zaidi ya sita vilivyo karibu na Mecúa. Wanafanya pia kazi kwenye shamba lao jipya kwa ajili ya kujikimu, na wakati huohuo wanatekeleza miradi miwili mikubwa: yaani ujenzi wa kanisa na kituo cha afya. Katika siku za usoni, jumuiya italazimika kuelekeza macho yake katika sekta ya elimu – sekta ambayo jamii inayozunguka Mecúa kwa hakika inahitaji msaada.

Wakati tunafurahia misioni hii na ushiriki wa ndugu zetu kutoka Tanzania, tunaamini kwamba mafanikio ya baadaye ya misioni hii yatategemea miito ya ndani ya nchi. Kwa sababu hii, tuko tayari na tutaendelea kuwa wazi kupokea maombi ya vijana wanaonesha nia, kuchambua nia hizi na kuwaandalia uwezekano wa kujiunga na maisha yetu ya kimonaki na kimisionari.