Abasia
Wito Wetu | Abasia

Wito Wetu

Wito Wetu

Abbey / Jumuiya / Wito Wetu

KIMSINGI  sisi tunajisikia kuitwa kuwa wamonaki walio  pia ni wamisionari. Wito wetu, pamoja na mambo mengine ni:

  • Kuishi roho ya kitawa na kimonaki kadiri ya mafundisho ya mwanzilishi wetu Mt. Benedikto,
  • Kuishi na kushirikisha tunu za Injili wale wote ambao tunaishi au kukutana nao katika maisha ya kila siku. Hapa tunajitahidi kutoa huduma za kichungaji (kiroho) bila kusahamu huduma nyinginezo za kibinadamu katika ujumla wake.
  • Kushiriki kikamilifu katika utume wa Kanisa wa kueneza Habari Njema kwa watu wote – iwe hapa nchini kwetu au hata nje ya nchi ikibidi.