Abasia
Ufundi Magari | Abasia
Ufundi Magari
Ufundi Magari
Abbey / Kazi Zetu / Ufundi Magari

WAMISIONARI walipofika Afrika mara ya kwanza changamoto yao kubwa ilikuwa ni usafiri. Kwanza walianza kutumia punda wa wapagazi. Pole pole, lakini, magari yalianza kutumika. Kilichofuata ni uhitaji wa mafundi magari na mahali pa kutengenzea magari hayo. Karakana ya kutengeneza magari ya Ndanda ikazaliwa. Kinyume na siku za nyuma, karakana hii inahudumia magari ya taasisi za aina zote pamoja na watu binafsi. Mafundi wazuri wenye kubobea wanahakikisha kuwa kila gari linalokuja kwetu linapona na kurudi barabarani tena. Karakana hii ni kitengo muhimu pia, sio tu kutoa ajira, bali pia kufundisha vijana wadogo katika maswala yote ya mahari.