Abasia
Ushonaji | Abasia

Ushonaji

Ushonaji

Abbey / Kazi Zetu / Ushonaji

MT. BENEDIKTO anawaasa watawa wake kuhakikisha kwamba kila kitu wanachohitaji kinapatikana ndani ya monastery. Aliamini kwamba si vyema watawa kutembea huko na huko kujitafutia mahitaji yao ya kila siku. Pengine hii inaeleza ni kwa sababu gani Wabenediktini wanakuwa na majengo mengi yenye shughuli lukuki ndani yake. Katika majengo yetu, ni karakana moja ambayo inajishusisha na ushonaji wa nguo. Miaka ya karibuni idara hii imekuwa na hadhi ya shule kwa viwango vya VETA. Hii inamaana kwamba vijana wanaweza kujiunga na idara hii, kujifunza ushonaji kwa miaka mitatu na kufanya mitihani ya taifa. Kwa sababu hiyo idara hii si kwa ajili ya ushonaji tu. Ni shule pia.