Abbey / Kazi Zetu / Uchapishaji Vitabu
KIWANDA CHA UCHAPISHAJI cha Ndanda (Ndanda Mission Press) kilianzishwa kwa lengo la kuchapisha vitabu vyenye lengo la kusaidia uinjilishaji. Leo, lakini, NMP inachapisha aina zote za vitabu – vya kidini na visivyo vya kidini. Vitabu vya hadithi, na hata vile vya kiada kwa ajili ya mashuleni – vyote vinaweza kuchapishwa na NMP. Licha ya vitabu NMP inatengeneza aina zote za madaftari kwa ajili ya mashuleni na maofisini. Na kama iliyo kawaida ya sekta zetu zingine, NMP ni mwajiri mzuri wa majirani zetu pamoja na kutoa nafasi ya vijana kujifunza maswala yote ya uchapishaji na “book-binding.”