Abasia
N’nango, Msumbiji | Abasia

N’nango, Msumbiji

Awasse, Msumbiji

Abbey / Umisionari / N’nango, Msumbiji

ABASIA YA NDANDA ni sehemu ya familia kubwa ya kimataifa ambayo ni Shirika la Wamisionari Wabenediktini wa Mt. Otilia. Hii ndio kusema kwamba kimsingi sisi ni jumuiya ya kimisionari. Katika kutambua wito wetu huo, mwaka 2014 tuliamua kufungua misioni mpya huko N’nango, kaskazini ya Msumbiji. Monasteri hii inayokua imewekwa chini ya Mt. Pakomio kama mlinzi na msimamizi wake. Lengo la kufungua misioni hii ni pamoja na:

  • Kwa kushirikiana na kanisa la Msumbiji kuimarisha Imani ya Kikiristu,
  • Kushirikiana na viongozi wa Kanisa, Kijamii na Kiserikali katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika jamii. Tungependa kutoa kipaumbele hapa katika elimu na malezi ya vijana pamoja na huduma za kiafya.
  • Kusimika na kueneza tunu za Kibenediktini kama mchango wetu katika kuimarisha Kanisa mahalia. Njia mojawapo ya kutekeleza hili ni kusimika maisha ya Kibenediktini ambayo msingi wake ni kuishi maisha ya sala na kazi kadiri ya Kanuni ya Mt. Benedikto. Kwa njia ya maisha yetu tunategemea kuweza kutoa mchango wetu katika kukuza Imani pamoja na kukabiliana na changamoto za kijamii na za kiuchumi zilizopo.