Abasia
Liturjia | Abasia

Liturjia

Liturjia

Abbey / Jumuiya / Liturjia

KAULI MBIU ya Maisha yetu ni SALA NA KAZI (Ora et Labora kwa Kilatini). Sala na Kazi ndio nguzo mbili muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Tunaanza siku kwa sala za pamoja, tunaenda kazini na kisha kurudi na kusali tena kwa pamoja mchana au jioni. Adhimisho la Ekaristi ni kilele cha sala zetu za kila siku. Mtindo wetu wa kusali ni wa pekee kwani tofauti na mashirika yaliyo mengi, sala zetu huimbwa daima kwa mtindo wa pekee ujulikano kama Gregorian Chant. Huu ni mtindo wa kuimba kadiri ulivyopangwa na Mt. Gregori. Kwa kawaida mashirika yasiyo ya kimonaki kama sisi hawatumiii mtindo huu wa kusali